Ruka hadi maudhui
Smart Invite

Smart Invite

Mialiko ya kidijitali kwa kila tukio

“Kila Tukio Lina Kadi Yake.”

Harusi, send-off, ubatizo, kipaimara, mahafali, makongamano na kadi za Krismasi — tengeneza kwa dakika chache, tuma kwa WhatsApp au SMS, na ujue nani anakuja.

Bure kuanza · Hakuna programu ya kupakua kwa wageni · Lipa unapotuma kwa wingi

Violezo Vinavyopendwa Zaidi

Miundo maridadi kwa harusi, ibada, sherehe na mikutano

Tiketi — ShereheSiku ya Kuzaliwa

Tiketi — KongamanoKongamano

Rangi za Maji — BluuUbatizo

Rangi za Maji — WaridiHarusi

Kitenge — Send-offSend-off

Kitenge — IndigoHarusi

Dhahabu — Usiku wa TuzoHafla ya Tuzo

Dhahabu ya ZumaridiMaadhimisho ya Ndoa

Dhahabu NyeusiHarusi

Polaroid — Kitchen PartyKitchen Party

Polaroid — KumbukumbuMkutano wa Familia

Herufi Kubwa — UzinduziUzinduzi wa Bidhaa

Herufi Kubwa — ChungwaSiku ya Kuzaliwa

Kioo — KongamanoKongamano

Tazama Violezo Vyote

Miundo 81 inakusubiri

Tengeneza mialiko ya kidijitali & simamia wageni

Tunza desturi · Furahia urahisi

  1. Hatua 1

    Chagua Kiolezo

    Miundo mizuri ya harusi, kanisa, sherehe na biashara.

  2. Hatua 2

    Jaza Maelezo Yako

    Ongeza picha, majina, tarehe, ukumbi, ratiba na ramani.

  3. Hatua 3

    Tuma Mwaliko

    Kwa WhatsApp, SMS, QR au kiungo — mgeni anafungua kwenye simu bila programu.

Tuko hapa unapotuhitaji

Msaada kwa Kiswahili na Kiingereza — kuanzia kuchagua kiolezo hadi kutuma kwa wageni.

Wageni & RSVP

Jua nani anakuja, panga kwa amani

Hakuna tena kupitia magrupu ya WhatsApp kuhesabu nani amethibitisha. Kila mgeni anapata kiungo chake, na majibu yanakuja mahali pamoja.

  • Ongeza wageni mmoja mmoja au pakia Excel/CSV, kisha wapange kwa makundi (familia, kamati, kanisa, VIP)
  • Kiungo binafsi kwa kila mgeni chenye jina lake na salamu — bila kuonyesha namba za simu
  • Wageni wanathibitisha: nitakuja, sitakuja au sina uhakika — pamoja na idadi na maswali yako
  • Tiketi za QR na check-in mlangoni kwa wasaidizi wako
  • Takwimu za moja kwa moja: waliotumiwa, waliojibu, wanaokuja
Badilisha muundo kwa uhuru

Badilisha muundo bila kuandika upya

Chagua muundo mwingine wakati wowote. Majina, wazazi, tarehe, ukumbi na picha zako zinabaki kama ulivyoziacha — muundo tu ndio unabadilika.

  • Ulichoandika kinabaki — hutaanza upya.
  • Badilisha mara nyingi upendavyo, bila gharama.
  • Kiungo ulichotuma hakibadiliki; wageni wanaona toleo jipya kila mara.
Mnakaribishwa kwenye harusi ya
Neema&Baraka

Kwa furaha kubwa tunakualika kushuhudia siku yetu ya baraka.

Jumamosi
12
Desemba
2026 · Saa 14:00
Kanisa la Mt. Petro Oysterbay, Dar es Salaam

Lugha

Kiswahili kwanza, Kiingereza pia

Andika mwaliko kwa Kiswahili, Kiingereza au zote mbili — inafaa kwa familia zenye wageni kutoka nje. Majina na ujumbe wako hayatafsiriwi kiotomatiki.

  • Maneno ya mwaliko (tarehe, saa, ukumbi) kwa lugha uliyochagua
  • Msaidizi wa AI wa hiari kupendekeza au kutafsiri ujumbe — wewe unaidhinisha
  • Tarehe kwa mtindo wa Kitanzania: Jumamosi, 12 Desemba 2026
KiswahiliEnglishLugha zaidi zinakuja
WhatsApp & SMS

Tuma kwa wageni wote kwa mbofyo mmoja

Kila mgeni anapokea ujumbe wenye jina lake na kiungo chake binafsi — kupitia WhatsApp Business rasmi au SMS ya kawaida kwa wasio na intaneti.

  • Unaona gharama kamili kabla ya kuthibitisha kutuma
  • Panga kutuma baadaye — hata kompyuta yako ikiwa imezimwa
  • Ripoti ya kweli: imepokelewa, imefika, imesomwa (pale mtoa huduma anaporipoti)
  • Ukumbusho wa RSVP kwa wasiojibu tu
  • Wageni wanaweza kujiondoa — tunaheshimu chaguo lao

Kushiriki mwenyewe kwa WhatsApp au kiungo ni bure kila wakati.

Kadi za salamu

Kadi za salamu kwa kila msimu

Krismasi, Pasaka, Eid, Mwaka Mpya, siku ya kuzaliwa, pole na asante — weka jina la kila mpokeaji na utume kwa wote kwa pamoja.

Kadi zote
Mpendwa Fatma
Eid Mubarak

Mwenyezi Mungu akubariki wewe na familia yako katika sikukuu hii njema.

Familia ya Salim
Mpya

Eid — Rangi za Maji

Eid

19
Juma
Happy Birthday!
Mwaka mpya wa maisha yako ujae baraka, afya na kicheko.
— Rafiki yako
Mpya

Heri ya Kuzaliwa — Herufi Kubwa

Heri ya Siku ya Kuzaliwa

Mpendwa Mgeni wetu
Asante Sana

Kwa kuja kwako, michango na maombi yako — siku yetu ilikamilika kwa sababu yako.

Neema & Baraka
Mpya

Asante — Mchoro

Asante

Amina
Heri ya 2027

Mwaka mpya uwe wa afya, mafanikio na furaha tele kwako na wapendwa wako.

KutokaFamilia ya Mushi
Mpya

Mwaka Mpya — Kioo

Mwaka Mpya

Mpendwa Amina
Krismasi Njema

Tunakutakia wewe na familia yako amani, furaha na baraka tele.

Familia ya Mushi
Mpya

Krismasi — Dhahabu Nyeusi

Krismasi

H
MpendwaHalima
Nakuwaza

Ujumbe mfupi kukukumbusha kwamba wewe ni wa thamani.

Kutoka kwa
Rafiki yako
Mpya

Salamu ya Kawaida

Salamu Nyingine

Kilele Holdings
MpendwaMteja wetu
Salamu za Msimu

Asante kwa kuendelea kutuamini. Tunakutakia sikukuu njema na mwaka wenye mafanikio.

Kutoka kwa
Timu ya Kilele
Mpya

Salamu za Msimu — Biashara

Salamu za Kibiashara

MpendwaMwalimu Salma
Tunathamini Mchango Wako

Asante kwa kujitoa kwako na moyo wako wa huduma.

Kutoka kwa
Uongozi
Mpya

Pongezi na Shukrani

Pongezi na Shukrani

Kila Unachohitaji

Mwaliko mmoja wenye kila kitu tukio lako linahitaji

Inafaa kwa Simu

Inafunguka vizuri kwenye simu yoyote, hata kwa intaneti ndogo.

Violezo Maridadi

Kuanzia kanga ya kitamaduni hadi muundo wa kisasa.

Ramani ya Google

Wageni wanafika ukumbini kwa mbofyo mmoja.

Albamu ya Picha

Onyesha picha zenu bora ndani ya mwaliko.

Kitabu cha Wageni

Wageni wanaacha salamu na pongezi zao.

Zawadi na Michango

Weka maelezo ya M-Pesa, Tigo Pesa au benki kwa michango.

QR na Check-in

Tiketi ya QR kwa kila mgeni na kuzuia kuingia mara mbili.

Pakua Picha na PDF

Kwa status, Instagram Story au kuchapisha.

Ratiba ya Tukio

Ibada, picha, chakula, burudani — kila kitu kwa saa yake.

Bei wazi, bila mshangao

Anza bure. Lipa kifurushi unapohitaji zaidi. Ujumbe wa WhatsApp/SMS unalipiwa kwa salio — unaona gharama kabla ya kutuma.

Bure

Bure

  • Mwaliko 1 au kadi 1
  • Violezo vya bure
  • Kiungo cha kushiriki + QR
  • RSVP hadi wageni 50
Anza bure

Tukio Moja

TSh 25,000 / mara moja

  • Violezo vyote (premium)
  • Wageni hadi 500 na viungo binafsi
  • Check-in kwa QR
  • Pakua PNG na PDF
Chagua
Inayopendwa

Kifurushi cha Harusi

TSh 75,000 / mara moja

  • Kila kitu cha Tukio Moja
  • Matukio 3 (send-off, kitchen party, harusi)
  • Salio la ujumbe TSh 30,000
  • Wageni hadi 1,500
Chagua

Mpangaji wa Matukio

TSh 150,000 / mwezi

  • Matukio 30 kwa mwezi
  • Wasaidizi wa check-in bila kikomo
  • Salio la ujumbe TSh 50,000 kila mwezi
  • Msaada wa kipaumbele
Chagua

Kanisa na Taasisi

TSh 1,200,000 / mwaka

  • Matukio na kadi za mwaka mzima
  • Kadi za msimu kwa waumini/wanachama wote
  • Salio la ujumbe TSh 300,000
  • Nembo yako kwenye kila kadi
Chagua

Bei kwa Shilingi za Tanzania. Ujumbe wa WhatsApp/SMS unakatwa kwenye salio lako kwa kiwango kinachoonyeshwa kabla ya kutuma.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Ni ukurasa mzuri wa mtandaoni wenye maelezo yote ya tukio lako — majina, tarehe, ukumbi, ramani, ratiba na fomu ya RSVP. Unatumwa kwa kiungo, na mgeni anaufungua kwenye simu bila kupakua programu.

Chagua kiolezo, jaza maelezo, badilisha rangi au picha ukipenda, kisha bofya Chapisha. Utapata kiungo cha kudumu na QR mara moja.

Kuanza ni bure. Vifurushi vya ziada (violezo premium, wageni wengi, check-in) na salio la WhatsApp/SMS vina bei zinazoonyeshwa wazi kwenye ukurasa wa Bei.

Kwa WhatsApp, SMS, barua pepe, QR iliyochapishwa au kiungo unachoshiriki popote. Kila mgeni anaweza kupata kiungo chake binafsi.

Hapana. Violezo vimeandaliwa tayari — unaandika maneno yako tu.

Majina ya wahusika na wazazi/wenyeji, tarehe na saa, ukumbi na ramani, ujumbe, ratiba, mavazi, mtu wa mawasiliano na orodha ya wageni yenye namba za simu.

Ndiyo, wakati wowote. Kiungo hakibadiliki na wageni wanaona toleo jipya mara moja.

Kiungo cha jumla hakina kikomo. Orodha ya wageni yenye viungo binafsi inategemea kifurushi chako.

Tukio lako linastahili kadi nzuri

Anza sasa — ni bure, na mwaliko wa kwanza uko tayari kwa dakika 5.